Mkuu wa Wilaya ya Morogoro (Mhe. Bakari Msulwa) akiwa ndiye Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Shirika lisilo la kiserikali, lisilo la faida la Youth Power Organization uliofanyika Siku ya jumapili tarehe 31/01/2021, Pamoja na tukio la Uzinduzi wa Shirika la Youth Power Organization, Mhe Bakari Msulwa ametoa pongezi Kwa Vijana wa Youth Power Organization ya kuwa ” Wamekuja na muelekeo mpya wa kuwawezesha na kuwajengea fikra vijana kujiajiri zaidi na si kufikiri kuajiriwa zaidi na Serikali. Haswa kwa kuwa Shirika lina muda mfupi tangu kusajiriwa kwake rasmi tare
he 05/01/2021 lakini Shirika lina mipango mizuri katika mambo ya Kilimo, Afya, Ufugaji, Viwanda, Ujasiriamali na Mazingira. Na kupitia Shirika hili vijana wameweka nguvu ya pamoja yakutumia taaluma yao kujiajiri na kuajiri wengine “.
Mhe Bakari Msulwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro ameahidi ” Serikali ipo tayari kutoa kila aina ya msaada kwa vijana popote pale walipo haswa kwa wale kupitia Shirika la Youth Power Organization. Ametoa Rai Kwa Youth Power Organization kujipanga na kuona maeneo gani Shirika linahitaji kuwekeza na Serikali itawasaidia na kuwaunga mkono. Ametoa wito Kwa Vijana wote wa Morogoro na kote nchini kuondokana na fikra kuwa Maisha ni kuajiriwa pekee yake.
Kwa sababu hiyo ndio Sera ya Taifa “Ujamaa na Kujitegemea”. Vijana watumie Shirika la Youth Power Organization kuweza kupata fursa zitakazowawezesha kujiajiri.
Wageni Maalumu pia walikuepo na walitoa Michango yao kwa Vijana. Miongoni mwa wageni hao ni Mhe. Dennis Lazaro Londo-Mbunge wa Mikumi na Mhe. Hamis Shabani Taletale (Babu Tale) Mbunge wa Morogoro Mashariki na Wageni Waalikwa Prof Mombo, Dr Lamtane kutoka SUA, Dr Lymo, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Kata ya Sultan Area na wengine wengi.
Wageni wote walionyesha nia kubwa ya kuwasaidia Vijana katika kubadilisha maisha yao na kuchochea Maendeleo ya Taifa kiujumla. Na wakatoa wito kwa vijana wote nchini kujiunga na Shirika la Youth Power Organization.

Leave a comment
Share a thought, ask a question, or add your perspective.
0 comments
Leave a commentBe the first to share a thought.